Posts

Showing posts from June, 2023

NJIA YA MSALABA KATIKA BIBLIA

    NJIA YA MSALABA KATIKA BIBLIA Kabla ya kila kituo: K: Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru; W: Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu. Baada ya kila kituo: 'Baba Yetu, 'Salamu Maria' na 'Atukuzwe Baba', K: Ee Bwana utuhurumie! W: Utuhurumie! K: Roho za waamini marehemu, wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. W: Amina (Kutoka “NJIA YA MSALABA INAYAGOMBEA KATIKA BIBLIA” - kimetungwa na Pdr. Thadei A. Mworia, OSS (Tabora, Tanzania) SALA YA KUFUNGUA Yesu akaenda pamoja na wanafunzi wake bustanini Gethsemane, akawaambia, "Kaeni hapa nami niendc pale mbele kusali". Akawachukua Petra na wana wawil wa Zebedayo, akaanza kuwa na huzuni na mahangaiko Hapo akawaambia, “'Nina huzuni kubwa moyoni hate karibu ya kufa. Kaeni hapa mkeshe pamoja nami". Basi, akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akasali, "Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki cha mateso kinipitie; lakini isiwe nitakavyo mimi, ila utakavyo wewe". (Mt 26:36-...

KITUO CHA KWANZA

Image
KITUO CHA KWANZA    YESU ANAHUKUMIWA AFE P: Kuhani Mkuu akamwuliza tena. "Je, wewe ndiye Masiha, Mwana wa Mungu Mtukufu?” Yesu akajibu, "Naam, mimi ndiye. Tena, mtamwona Mwana wa Mtu amekaa upande wa kulia wa Mwenye Nguvu, akija katika mawingu ya mbinguni”. Hapo Kuhani Mkuu akararua joho lake, akasema, Tuna haja gani tena ya mashahidi? Mmesikia kufuru yake! Ninyi mwaonaje?” Wote wakamua kwamba anastahili kuuawa. (Mk 14:61-64). W: Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, juu ya Bwana na juu ya Masiha wake, Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako na miisho ya dunia kuwa milki yako. (Zab 2:7-8). Tuombe: Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia kwa kutamka kuwa wewe ni Mwana wa Mungu umehukumiwa kufa bila kosa. Tufanye tusikuhukumu mara nyingine kufa kwa dhambi zetu bali kutokana na kifo chako tujaliwe ujasiri wa kukukiri wewe unayekaa upande wa Mwenye-enzi na kutawala daim...

KITUO CHA PILI

Image
  KITUO CHA PILI  YESU ANAPOKEA MSALABA P. Pilato akawaambia Wayahudi, "Tazameni mfalme wenu!' Wao wakapaaza sauti: "Mwondoe! Mwondoe! Msulibishe!' Pilato akawauliza, 'Je, nimsulibishe Mfalme wenu?' Makuhani wakuu wakajibu, "Sisi hatuna Mfalme isipokuwa Kaisari!” Basi, hapo Pilato akamtia Yesu mikononi mwao ili asulibiwe. Basi, wakamchukua Yesu. Naye akatoka akiwa amejichukulia msalaba wake kwenda mahali paitwapo, ‘Fuvu la Kichwa’ (Kwa Kiebrania Golgota) (Yn 19:14-17). W. Ni nani aliyesadiki habari tuliyoisikia? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? Maana alikuwa mbele zake kama mche mwororo Na kama mzizi katika nchi kavu. Yeye hana umbo wala uzuri Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. Alidharauliwa na kukataliwa na watu. Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao. Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu (Isa 53:1-3). Tuombe: Baba wa mbinguni, kwa kumkiri Mwanao Yesu Kristo, kaka na dada zake wanabebeshwa msalaba w...

KITUO CHA NNE

Image
KITUO CHA NNE YESU ANAKUTANA NA MAMA YAKE Ee Yesu Tunakuabudu, tunakushu; kwa kuwa umewakomboa watu kwa Msalaba wako Mtakatifu. Bila shaka kituo hiki kilikuwa chenye kuumiza na kusikitika kwa Maria Mama Huzuni, kumwangalia Mwanawe Mpendwa sana akilemewa na mzigo wa Msalaba! Moyo wake ulizoea maumivu mengi yasiyosemeka. Alitamani sana kufa badala ya Yesu au pamoja naye. Umsihi Mama huyu wa Huzuni akusaidie katika saa ya kufa kwako. Ee Yesu, ee Maria, mimi ni sababu ya maumivu mengi na makubwa ambayo yanachoma mioyo yenu! Moyo wangu pia uweze kuhisi na kozoea hata kidogo cha maumivu yenu. Ee Mama qa Huzuni, uniwezeshe kushiriki katika mateso uliyovumilia wewe na Mwanao kwa ajili yangu, na unijalie nizoee huzuni yako, ili nikiumizwa nayo niweze kufurahia msaada wako saa ya kifo changu. Baba Yetu...Salamu Maria...Atukuzwe Baba. TAFAKARI:- Katika kituo hiki inakutana Mioyo miwili mitakatifu lakini iliojaa Uchungu mwingi sana kwa ajili ya dhambi zetu. Mama Maria anahuzunika kutokana na mates...

KITUO CHA TATU

Image
  KITUO CHA TATU  YESU ANAANGUKA MARA YA KWANZA P. 'Kama ulimwengu ukiwachukia ninyi, kumbukeni kwamba umenichukia mimi kabla haujawachukia ninyi. Kama mngalikuwa watu wa ulimwengu, ulimwengu ungaliwapenda ninyi, watu wake. Lakini kwa vile ninyi si wa ulimwengu. ila mimi nimewachagueni kutoka ulimwenguni, kwa sababu hiyo ulimwengu unawachukieni. Kumbukeni niltyowaambieni: mtumishi si mkuu zaidi kuliko Bwana wake. Ikiwa wamenitesa mimi, watawatesa na ninyi pia; kama wameshika neno langu, watalishika na lenu pia. (Yn 15:18-20). W. Kwani mavazi yako kuwa mekundu, Na nguo zako kama za mtu akanyagaye zabibu? Nilikanyaga shinikizoni peke yangu; Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami; Naam, naliwakanyaga kwa hasira yangu, Naliwaponda kwa ghadhabu yangu; Na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao, Nami nimezichafua nguo zangu zote. Nikatazama, wala hakuna wa kunisaidia; Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza; Basi mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu, Ghadhabu yangu ndiyo...

KITUO CHA TANO

Image
  KITUO CHA TANO  SIMONI WA KIRENE ANABEBESHWA MSALABA AUCHUKUE NYUMA YA YASU P: Walipokuwa wanampeleka, walikutana na mtu mmoja, aitwaye Simoni wa Kirene, aliyekuwa anatoka mashambani. Basi, walimkamata, wakamtwisha ule msalaba auchukue nyuma yake Yesu. Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgota, maana yake "Mahali pa Fuvu la Kichwa" (Lk 23:26; Mk 15:21). W. Kwa sauti yangu nitamlilia Bwana, kwa sauti yangu nitamwomba Bwana dua. Nitafunua mbele zaka malalamiko yangu, shida yangu nitaitangaza mbele zake. Nilipozimia roho yangu uliyajua mapito yangu; Katika njia niendayo wamenifichia mtego. Utazama mkono wa kuume ukaone, kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipolea, hakuna wa kunitunza roho. Bwana nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu, Fungu langu katka nchi ya walio hai (Zab 141:1-5) Tuombe: Bwana Yesu, tunakutana na watu wanaoteseka ambao umewaweka katika njia tunayopita. Tufundishe kuwaonea huruma na tuwe tayari kuchukua pamoja nao msalaba wao. Amina

KITUO CHA SITA

Image
  KITUO CHA SITA  VERONIKA ANAUPANGUSA USO WA YESU P. Hapo, hao watu wema watamjibu mfalme: "Bwana, lini tulikuona mwenye njaa tukakupa chakula, au ukiwa na kiu tukakunywesha maji? Lini tulikuona ukiwa mgeni tukakukaribisha au bila nguo tukakuvika? Lini tulikuona ukiwa mgonjwa tukaja kukutazama?” Mfalme atawajibu: “Kweli nawaambieni, kila kitu mlichomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi" (Mt 25:37-40). W. Walakini rafiki aliye amini ndiye ngome; naye aliyempata amepata tunu. Hakuna badala ya rafiki amini, wala uzuri wake hauna bei. Rafiki amini ni kifunga uzima; naye amchaye Mungu atampata. Mcha Mungu hunyoosha urafiki wake, kwa maana alivyo yeye mwenyewe, ndivyo alivyo na jirani yake (YbS 6:14-17). Tuombe: Yesu, tufanye tuone uso wako ndani ya wanaoteseka. Katika mateso utufundishe upendo, utufundishe upendo hasa katika mateso. Amina

KITUO CHA SABA

Image
  KITUO CHA SABA  YESU ANAANGUKA MARA YA PILI P: Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhani ya kuwa amepigwa. Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Basi alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yatu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote (Isa 53:4-6). W. Alionewa, lakini alinyenyekea, wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana kondoo apelekwaye machinjioni, na kama vile kondoo anyamazavyo mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake. Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani atakayeyasimulia? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu (Isa 53:7-8). Tuombe: Ee Bwana Yesu, kuanguka kwako chini ya uzito wa msalaba ni kielelezo cha kuanguka kwetu chini ya uzito wa dhambi na makosa. Angaza dhamiri zetu tu...

KITUO CHA NANE

  KITUO CHA NANE   AKINA MAMA WANAMLILIA YESU P. Watu, umati kwa umati, walimfuata; miongoni mwao vakiwamo wanawake waliokuwa wanaomboleza na kumlilia. Yesu akawageukia, akasema, "Enyi akina mama wa Yerusalemu! Msinililie mimi, ila lieni kwa ajili yenu wenyewe na kwa ajili ya watoto wenu (Lk 23:27-28). W. Je si kitu kwenu, enyi nyote mpitao njia, Angalieni, mtazame kama kuna majonzi yoyote mfano wa majonzi yangu, Niliyotendwa mimi, ambayo Bwana amenihuzunisha kwa hayo. Siku za hasira yake iwakayo. Mimi ninayalilia mambo hayo; Jicho langu, jicho langu linachuruzika maji; kwa kuwa mfariji yu mbali nami, ambayo ilimpasa kunihuisha nafsi; Watoto wangu wameachwa poke yao, kwa sababu huyo adui ameshinda (Omb 1:12-16). Tuombe: Bwana Yesu, hawa wanawake wa Yerusalemu waliodondosha machozi ya huruma walipokuona njiani kwenda Kalvari umepigwa, umechubuliwa, umetobolewa na miiba. Ongeza imani yangu ili niweze kukuona katika ndugu yangu aliyepigwa kwa maneno yangu mabaya, aliyechubul...

KITUO CHA TISA

  KITUO CHA TISA  - YESU ANAANGUKA MARA YA TATU P. Nafsi yangu imeambatana na mavumbi, unihuisha sawasawa na neno lako. Nalizisimulia njia zangu ukanijibu, unifundisha amri zako. Unifahamisha njia ya mausia yako, nami nitayatafakari maajabu yako. Nafsi yangu imeyeyuka kwa uzito, unitie nguvu sawasawa na neno lako (Zab 119: 25-28). W. Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, nimhofu nani? Watanda mabaya waliponikaribia, wanile nyama yangu, watesi wangu na adui zangu, walijikwaa wakaanguka. Jeshi lijapojipanga kupigana nami. Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, hata hapo nitatumaini (Zab 27:1-3). Tuombe: Ee Yesu, kwa kuzidi kudhoofika kwa mateso unaanguka mara ya tatu chini ya msalaba. Tunakuomba, gusa kwa neema yako dhamiri zatu tupata kujua kweli ubaya wa dhambi ulizokuja kuondoa kwa mateso na ufufuko wako. Amina

KITUO CHA KUMI

  KITUO CHA KUMI 

KITUO CHA KUMI NA MOJA

KITUO CHA KUMI NA MOJA

KITUO CHA KUMI NA MBILI -

  KITUO CHA KUMI NA MBILI   YESU ANAKUFA MSALABANI P. Ilikuwa yapata saa sita mchana; jua likaacha kuangaza, giza likaivamia nchi yote mpaka saa tisa, na pazia lililokuwa limetundikwa Hekaluni likapasuka katikati. Yesu akalia kwa sauti kubwa: “Baba, mikononi nwako naiweka roho yangu”. Alipokwisha kusema hayo, akatoa roho. Jemadari na wale waliokuwa wakimchunga Yesu walipoona mtetemeko wa ardhi na yale mambo yaliyotukia, wakaogopa sana, wakasema, “kweli mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu” (Lk 23:44-46; Mt 27:54). W. Kabila langu, Nimekutendea nini? au kwa jambo gani nimekusikitisha? Nijibu ! 1. Mimi nimekukomboa kutoka nchi ya Misri, nawe ukamtengenezea mkombozi wako msalaba. 2. Mimi nimewapiga mijeledi Wamisri kwa ajili yako, nakamtoa mkombozi wako apigwe mijeledi. 3. Mimi nimeifunua bahari ya Sham mbele yako, nawe ukaufunua ubavu wangu kwa mkuki. 4. Mimi nimekulisha mana na maji jangwani, nawe ukaninywesha nyongo na siki. 5. Mimi nimewapiga wafalme wa Kanaani kwa ajili yako...

KITUO CHA KUMI NA TATU

  KITUO CHA KUMI NA TATU   YESU ANASHUSHWA MSALABANI P: Lakini walipomfikia Yesu waliona kwamba alikwisha kufa, na hivyo hawakumvunja miguu. Lakini askari mmoja akamtoboa ubavuni kwa mkuki na mara ikatoka damu na maji. Baada ya hayo, Yosefu, mwenyeji wa Arimataya, alimuomba Pilato ruhusa ya kuuchukua mwili wa Yesu. Basi Pilato akaamuru apawa (Yn 19:33-34,38; Mt 27:58). W. Basi tabiri uwaambie, Bwana Mungu asema hivi: Tazama, nitafunua makaburi yenu, na kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu, enyi watu wangu, nami nitawaingizeni katika nchi ya Waisraeli. Nanyi mtajua kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapoyafunua makaburi yenu na kuwatoa katika makaburi, enyi watu wangu, nami nitatia roho yangu ndani yenu, nanyi mtaishi, nami nitawawekeni katika nchi yenu, nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, nimesema hayo, na kuyatimiza asema Bwana. (Eze 37:12-14). Tuombe: Ee Yesu, ulimrudishia Baba yako wa mbinguni kila alichokupa. Nasi ukatupa kila kitu ulichokuwa nacho, hadi ukatoa uzima wako kwa aj...

KITUO CHA KUMI NA NNE

Image
 ✟  KITUO CHA KUMI NA NNE