KITUO CHA TATU
KITUO CHA TATU
YESU ANAANGUKA MARA YA KWANZA
P. 'Kama ulimwengu ukiwachukia ninyi, kumbukeni kwamba umenichukia mimi kabla haujawachukia ninyi. Kama mngalikuwa watu wa ulimwengu, ulimwengu ungaliwapenda ninyi, watu wake. Lakini kwa vile ninyi si wa ulimwengu. ila mimi nimewachagueni kutoka ulimwenguni, kwa sababu hiyo ulimwengu unawachukieni. Kumbukeni niltyowaambieni: mtumishi si mkuu zaidi kuliko Bwana wake. Ikiwa wamenitesa mimi, watawatesa na ninyi pia; kama wameshika neno langu, watalishika na lenu pia. (Yn 15:18-20).W. Kwani mavazi yako kuwa mekundu, Na nguo zako kama za mtu akanyagaye zabibu? Nilikanyaga shinikizoni peke yangu; Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami; Naam, naliwakanyaga kwa hasira yangu, Naliwaponda kwa ghadhabu yangu; Na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao, Nami nimezichafua nguo zangu zote. Nikatazama, wala hakuna wa kunisaidia; Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza; Basi mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu, Ghadhabu yangu ndiyo iliyonitegemeza (Isa 63:2,3,5).
Tuombe: Tunakushukuru Yesu kwa kutuchagua kuendeleza kazi ya ukombozi wa binadamu. Tukianguka ututie shime tuamke, tusimame mara kutumikia watu wote hata kama dunia inatuchukia. Amina

Comments
Post a Comment