Posts

NJIA YA MSALABA KATIKA BIBLIA

    NJIA YA MSALABA KATIKA BIBLIA Kabla ya kila kituo: K: Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru; W: Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu. Baada ya kila kituo: 'Baba Yetu, 'Salamu Maria' na 'Atukuzwe Baba', K: Ee Bwana utuhurumie! W: Utuhurumie! K: Roho za waamini marehemu, wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. W: Amina (Kutoka “NJIA YA MSALABA INAYAGOMBEA KATIKA BIBLIA” - kimetungwa na Pdr. Thadei A. Mworia, OSS (Tabora, Tanzania) SALA YA KUFUNGUA Yesu akaenda pamoja na wanafunzi wake bustanini Gethsemane, akawaambia, "Kaeni hapa nami niendc pale mbele kusali". Akawachukua Petra na wana wawil wa Zebedayo, akaanza kuwa na huzuni na mahangaiko Hapo akawaambia, “'Nina huzuni kubwa moyoni hate karibu ya kufa. Kaeni hapa mkeshe pamoja nami". Basi, akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akasali, "Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki cha mateso kinipitie; lakini isiwe nitakavyo mimi, ila utakavyo wewe". (Mt 26:36-...

KITUO CHA KWANZA

Image
KITUO CHA KWANZA    YESU ANAHUKUMIWA AFE P: Kuhani Mkuu akamwuliza tena. "Je, wewe ndiye Masiha, Mwana wa Mungu Mtukufu?” Yesu akajibu, "Naam, mimi ndiye. Tena, mtamwona Mwana wa Mtu amekaa upande wa kulia wa Mwenye Nguvu, akija katika mawingu ya mbinguni”. Hapo Kuhani Mkuu akararua joho lake, akasema, Tuna haja gani tena ya mashahidi? Mmesikia kufuru yake! Ninyi mwaonaje?” Wote wakamua kwamba anastahili kuuawa. (Mk 14:61-64). W: Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, juu ya Bwana na juu ya Masiha wake, Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako na miisho ya dunia kuwa milki yako. (Zab 2:7-8). Tuombe: Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia kwa kutamka kuwa wewe ni Mwana wa Mungu umehukumiwa kufa bila kosa. Tufanye tusikuhukumu mara nyingine kufa kwa dhambi zetu bali kutokana na kifo chako tujaliwe ujasiri wa kukukiri wewe unayekaa upande wa Mwenye-enzi na kutawala daim...

KITUO CHA PILI

Image
  KITUO CHA PILI  YESU ANAPOKEA MSALABA P. Pilato akawaambia Wayahudi, "Tazameni mfalme wenu!' Wao wakapaaza sauti: "Mwondoe! Mwondoe! Msulibishe!' Pilato akawauliza, 'Je, nimsulibishe Mfalme wenu?' Makuhani wakuu wakajibu, "Sisi hatuna Mfalme isipokuwa Kaisari!” Basi, hapo Pilato akamtia Yesu mikononi mwao ili asulibiwe. Basi, wakamchukua Yesu. Naye akatoka akiwa amejichukulia msalaba wake kwenda mahali paitwapo, ‘Fuvu la Kichwa’ (Kwa Kiebrania Golgota) (Yn 19:14-17). W. Ni nani aliyesadiki habari tuliyoisikia? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? Maana alikuwa mbele zake kama mche mwororo Na kama mzizi katika nchi kavu. Yeye hana umbo wala uzuri Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. Alidharauliwa na kukataliwa na watu. Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao. Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu (Isa 53:1-3). Tuombe: Baba wa mbinguni, kwa kumkiri Mwanao Yesu Kristo, kaka na dada zake wanabebeshwa msalaba w...

KITUO CHA NNE

Image
KITUO CHA NNE YESU ANAKUTANA NA MAMA YAKE Ee Yesu Tunakuabudu, tunakushu; kwa kuwa umewakomboa watu kwa Msalaba wako Mtakatifu. Bila shaka kituo hiki kilikuwa chenye kuumiza na kusikitika kwa Maria Mama Huzuni, kumwangalia Mwanawe Mpendwa sana akilemewa na mzigo wa Msalaba! Moyo wake ulizoea maumivu mengi yasiyosemeka. Alitamani sana kufa badala ya Yesu au pamoja naye. Umsihi Mama huyu wa Huzuni akusaidie katika saa ya kufa kwako. Ee Yesu, ee Maria, mimi ni sababu ya maumivu mengi na makubwa ambayo yanachoma mioyo yenu! Moyo wangu pia uweze kuhisi na kozoea hata kidogo cha maumivu yenu. Ee Mama qa Huzuni, uniwezeshe kushiriki katika mateso uliyovumilia wewe na Mwanao kwa ajili yangu, na unijalie nizoee huzuni yako, ili nikiumizwa nayo niweze kufurahia msaada wako saa ya kifo changu. Baba Yetu...Salamu Maria...Atukuzwe Baba. TAFAKARI:- Katika kituo hiki inakutana Mioyo miwili mitakatifu lakini iliojaa Uchungu mwingi sana kwa ajili ya dhambi zetu. Mama Maria anahuzunika kutokana na mates...

KITUO CHA TATU

Image
  KITUO CHA TATU  YESU ANAANGUKA MARA YA KWANZA P. 'Kama ulimwengu ukiwachukia ninyi, kumbukeni kwamba umenichukia mimi kabla haujawachukia ninyi. Kama mngalikuwa watu wa ulimwengu, ulimwengu ungaliwapenda ninyi, watu wake. Lakini kwa vile ninyi si wa ulimwengu. ila mimi nimewachagueni kutoka ulimwenguni, kwa sababu hiyo ulimwengu unawachukieni. Kumbukeni niltyowaambieni: mtumishi si mkuu zaidi kuliko Bwana wake. Ikiwa wamenitesa mimi, watawatesa na ninyi pia; kama wameshika neno langu, watalishika na lenu pia. (Yn 15:18-20). W. Kwani mavazi yako kuwa mekundu, Na nguo zako kama za mtu akanyagaye zabibu? Nilikanyaga shinikizoni peke yangu; Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami; Naam, naliwakanyaga kwa hasira yangu, Naliwaponda kwa ghadhabu yangu; Na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao, Nami nimezichafua nguo zangu zote. Nikatazama, wala hakuna wa kunisaidia; Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza; Basi mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu, Ghadhabu yangu ndiyo...

KITUO CHA TANO

Image
  KITUO CHA TANO  SIMONI WA KIRENE ANABEBESHWA MSALABA AUCHUKUE NYUMA YA YASU P: Walipokuwa wanampeleka, walikutana na mtu mmoja, aitwaye Simoni wa Kirene, aliyekuwa anatoka mashambani. Basi, walimkamata, wakamtwisha ule msalaba auchukue nyuma yake Yesu. Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgota, maana yake "Mahali pa Fuvu la Kichwa" (Lk 23:26; Mk 15:21). W. Kwa sauti yangu nitamlilia Bwana, kwa sauti yangu nitamwomba Bwana dua. Nitafunua mbele zaka malalamiko yangu, shida yangu nitaitangaza mbele zake. Nilipozimia roho yangu uliyajua mapito yangu; Katika njia niendayo wamenifichia mtego. Utazama mkono wa kuume ukaone, kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipolea, hakuna wa kunitunza roho. Bwana nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu, Fungu langu katka nchi ya walio hai (Zab 141:1-5) Tuombe: Bwana Yesu, tunakutana na watu wanaoteseka ambao umewaweka katika njia tunayopita. Tufundishe kuwaonea huruma na tuwe tayari kuchukua pamoja nao msalaba wao. Amina

KITUO CHA SITA

Image
  KITUO CHA SITA  VERONIKA ANAUPANGUSA USO WA YESU P. Hapo, hao watu wema watamjibu mfalme: "Bwana, lini tulikuona mwenye njaa tukakupa chakula, au ukiwa na kiu tukakunywesha maji? Lini tulikuona ukiwa mgeni tukakukaribisha au bila nguo tukakuvika? Lini tulikuona ukiwa mgonjwa tukaja kukutazama?” Mfalme atawajibu: “Kweli nawaambieni, kila kitu mlichomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi" (Mt 25:37-40). W. Walakini rafiki aliye amini ndiye ngome; naye aliyempata amepata tunu. Hakuna badala ya rafiki amini, wala uzuri wake hauna bei. Rafiki amini ni kifunga uzima; naye amchaye Mungu atampata. Mcha Mungu hunyoosha urafiki wake, kwa maana alivyo yeye mwenyewe, ndivyo alivyo na jirani yake (YbS 6:14-17). Tuombe: Yesu, tufanye tuone uso wako ndani ya wanaoteseka. Katika mateso utufundishe upendo, utufundishe upendo hasa katika mateso. Amina