KITUO CHA KUMI NA NNE

 ✟ KITUO CHA KUMI NA NNE

 YESU ANAZIKWA KABURINI

P: Yosefu akauchukua ule mwili akauzungushia sanda safi ya kitani, akauweka ndani ya kaburi lake jipya alilokuwa amelichonga katika mwamba. Kisha akaviringisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake. Wale wanawake walioandamana na Yesu toka Galilaya w

akaliona lile Kaburi na jinsi mwili wake Yesu ulivyowekwa. Halafu walirudi nyumbani kwao, wakawa wanayatayarisha manukato na marashi kwa ajili ya mwili wake (Mt 27:59-60; Lk 23:55-56).


W: Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya; Na pamoja na matajiri katika kufa kwake: Ingawa hakutenda jeuri, wala hapakuwa na hila kinywani mwake. Lakini Bwana aliridhika kumchubua: Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake: Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki. Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao. Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu. Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa. Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji (Isa 53:9-12).

Tuombe: Kaburi lako Yesu linaficha ndani yake fumbo la chanzo cha uzima mpya. Kila siku tunatembea kuelekea kaburi letu. Tunaomba uzima uliotoka katika kaburi lako siku ile ya ufufuko uwe mwanga kwetu tunapotembea hapa duniani ili nasi siku ya mwisho tufufukie huo uzima mpya. Amina

SALA YA MWISHO
Yesu wangu, kwa uchungu wote ulioona juu ya msalaba, na kwa kuzimia kwako kwa ukali wa mateso, unijalie nguvu ya kuvumilia kwa moyo taabu zote sasa na saa ya kuzimia kwangu. Nawe Maria Mamangu, kwa uchungu wote ambao moyo wako umejaa ulipomwona Mwanao mpenzi kuinama kichwa na kuzimia, unifadhili nife kifo chema.

Comments

Popular posts from this blog

NJIA YA MSALABA KATIKA BIBLIA

NJIA YA MSALABA

KITUO CHA KWANZA