KITUO CHA SABA
KITUO CHA SABA
YESU ANAANGUKA MARA YA PILI
P: Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhani ya kuwa amepigwa. Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Basi alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yatu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote (Isa 53:4-6).W. Alionewa, lakini alinyenyekea, wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana kondoo apelekwaye machinjioni, na kama vile kondoo anyamazavyo mbele yao wakatao manyoya yake;
Naam, hakufunua kinywa chake. Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani atakayeyasimulia? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu (Isa 53:7-8).
Tuombe: Ee Bwana Yesu, kuanguka kwako chini ya uzito wa msalaba ni kielelezo cha kuanguka kwetu chini ya uzito wa dhambi na makosa. Angaza dhamiri zetu tuone udhaifu wetu. Tupe nguvu ya kutubu kwa dhati tusirudie tena dhambi. Amina

Comments
Post a Comment