KITUO CHA NNE



KITUO CHA NNE

YESU ANAKUTANA NA MAMA YAKE

Ee Yesu Tunakuabudu, tunakushu; kwa kuwa umewakomboa watu kwa Msalaba wako Mtakatifu.

Bila shaka kituo hiki kilikuwa chenye kuumiza na kusikitika kwa Maria Mama Huzuni, kumwangalia Mwanawe Mpendwa sana akilemewa na mzigo wa Msalaba! Moyo wake ulizoea maumivu mengi yasiyosemeka. Alitamani sana kufa badala ya Yesu au pamoja naye. Umsihi Mama huyu wa Huzuni akusaidie katika saa ya kufa kwako. Ee Yesu, ee Maria, mimi ni sababu ya maumivu mengi na
makubwa ambayo yanachoma mioyo yenu! Moyo wangu pia uweze kuhisi na kozoea hata kidogo cha maumivu yenu. Ee Mama qa Huzuni, uniwezeshe kushiriki katika mateso uliyovumilia wewe na Mwanao kwa ajili yangu, na unijalie nizoee huzuni yako, ili nikiumizwa nayo niweze kufurahia msaada wako saa ya kifo changu.

Baba Yetu...Salamu Maria...Atukuzwe Baba.

TAFAKARI:- Katika kituo hiki inakutana Mioyo miwili mitakatifu lakini iliojaa Uchungu mwingi sana kwa ajili ya dhambi zetu. Mama Maria anahuzunika kutokana na mateso ya mwanae ambaye hana hatia. Ni dhambi zetu ambazo zinasababisha maumivu Haya. Lakini tutafakari jinsi gani Mama Maria, Mama wa Mateso mengi alivyo na upendo kwetu! Sisi ndio tunasababisha mwanaye mpendwa ateseke asulubiwe na afe kifo cha fedhea msalabani. Pamoja na kusababisha maumivu haya bado Mama Maria siku zote hutuombea kwa Mwanaye Yesu Kristo neema nyingi, ni upendo kiasi gani!? Anatufariji, anatupa amani, furaha n.k Ni wa kushangaza upendo wake. Tafakari je wewe unaweza kumuombea au kumsaidia mtu ambaye anasababisha maumivu kwako moja kwa moja au kupitia mtu wako wa karibu unayempenda? Wengi wetu hatuwezi kuvumilia. Basi tutafakari katika siku ya leo, ni dhambi zetu zipi ambazo zinaendelea kuumiza Mioyo ya Yesu na Maria, na tuombe neema ya Mungu kupitia kwa Mama Maria ili tuachane na dhambi hizo ambazo ni sababu ya maumivu kwa Yesu na Mama Maria.

SALA: Ee Yesu na Maria, nisaidie niweze kupata uchungu juu za dhambi zangu. Nijaze na huzuni ile ile mlioipata baada ya kukutana katika njia ya Msalaba ili nisiweze kutenda dhambi tena. Amia.

Comments

Popular posts from this blog

NJIA YA MSALABA KATIKA BIBLIA

NJIA YA MSALABA

KITUO CHA KWANZA