KITUO CHA TANO
KITUO CHA TANO
SIMONI WA KIRENE ANABEBESHWA MSALABA AUCHUKUE NYUMA YA YASU
P: Walipokuwa wanampeleka, walikutana na mtu mmoja, aitwaye Simoni wa Kirene, aliyekuwa anatoka mashambani. Basi, walimkamata, wakamtwisha ule msalaba auchukue nyuma yake Yesu. Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgota, maana yake "Mahali pa Fuvu la Kichwa" (Lk 23:26; Mk 15:21).W. Kwa sauti yangu nitamlilia Bwana, kwa sauti yangu nitamwomba Bwana dua. Nitafunua mbele zaka malalamiko yangu, shida yangu nitaitangaza mbele zake. Nilipozimia roho yangu uliyajua mapito yangu; Katika njia niendayo wamenifichia mtego. Utazama mkono wa kuume ukaone, kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipolea, hakuna wa kunitunza roho. Bwana nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu, Fungu langu katka nchi ya walio hai (Zab 141:1-5)
Tuombe: Bwana Yesu, tunakutana na watu wanaoteseka ambao umewaweka katika njia tunayopita. Tufundishe kuwaonea huruma na tuwe tayari kuchukua pamoja nao msalaba wao. Amina

Comments
Post a Comment