KITUO CHA PILI
KITUO CHA PILI
YESU ANAPOKEA MSALABA
P. Pilato akawaambia Wayahudi, "Tazameni mfalme wenu!' Wao wakapaaza sauti: "Mwondoe! Mwondoe! Msulibishe!' Pilato akawauliza, 'Je, nimsulibishe Mfalme wenu?' Makuhani wakuu wakajibu, "Sisi hatuna Mfalme isipokuwa Kaisari!” Basi, hapo Pilato akamtia Yesu mikononi mwao ili asulibiwe. Basi, wakamchukua Yesu. Naye akatoka akiwa amejichukulia msalaba wake kwenda mahali paitwapo, ‘Fuvu la Kichwa’ (Kwa Kiebrania Golgota) (Yn 19:14-17).W. Ni nani aliyesadiki habari tuliyoisikia? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? Maana alikuwa mbele zake kama mche mwororo Na kama mzizi katika nchi kavu. Yeye hana umbo wala uzuri Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. Alidharauliwa na kukataliwa na watu. Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao. Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu (Isa 53:1-3).
Tuombe: Baba wa mbinguni, kwa kumkiri Mwanao Yesu Kristo, kaka na dada zake wanabebeshwa msalaba wa mateso. Uwe nao wanaodhulumiwa na kudhalilishwa kwa ajili ya jina la Kristo, Bwana wetu. Amina.

Comments
Post a Comment