KITUO CHA TISA
KITUO CHA TISA
- YESU ANAANGUKA MARA YA TATU
P. Nafsi yangu imeambatana na mavumbi, unihuisha sawasawa na neno lako. Nalizisimulia njia zangu ukanijibu, unifundisha amri zako. Unifahamisha njia ya mausia yako, nami nitayatafakari maajabu yako. Nafsi yangu imeyeyuka kwa uzito, unitie nguvu sawasawa na neno lako (Zab 119: 25-28).W. Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, nimhofu nani? Watanda mabaya waliponikaribia, wanile nyama yangu, watesi wangu na adui zangu, walijikwaa wakaanguka. Jeshi lijapojipanga kupigana nami. Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, hata hapo nitatumaini (Zab 27:1-3).
Tuombe: Ee Yesu, kwa kuzidi kudhoofika kwa mateso unaanguka mara ya tatu chini ya msalaba. Tunakuomba, gusa kwa neema yako dhamiri zatu tupata kujua kweli ubaya wa dhambi ulizokuja kuondoa kwa mateso na ufufuko wako. Amina
Comments
Post a Comment